Kibor Elizabeth,
Nguzo Publication.
Mtu kasema kutoa ni moyo, usambe ni utajiri. Mwingine kanena tenda mema nenda zako. Haya yote bila shaka ni wengi hukubaliana nayo. Japo kwa bayana ni wachache ambao huambatanisha maneno haya na mienendo. Wengi utawapata wakiyatamka bali matendo yakidhihirika, huwa jambo gumu.
Mwanadamu ana mengi, baba mmoja aliyekuwa
na viumbe walioonekana kama ongezeko la nyama mwilini hakuwa na amani katu.
Kila aliyemuona alimuogopa na kumuepuka. Hili lilikuwa jambo ambalo lilimfanya kuhisi
kuchukiwa na wenzake. Hakuna aliyetaka kumsalimu au kumkaribia. Yule aliyekuwa
ameketi kando yake kwenye gari alikuwa akimkazia jicho pale ambapo angethubutu
kumgusa.
Japo baba huyu alionekana kana kwamba
amechipuka mwili wote, huu haukuonekana Kama ugonjwa wa kusambazwa wala haikuwa
jambo la kumfanya kuogofya. Watu walisababisha baba huyu kuhisi ukiwa badala ya
kumtendea wema wa kumuamkua, kupiga gumzo, na kumpa fursa ya kutangamana. Ama kweli
ya mwanadamu ni mengi, ya Mungu ni makuu.
Kwenye gari jingine, kukawa na utu, dada mmoja
ambaye alikuwa akiugua alializidiwa na moto kwenye gari na kutapika. Kwa bahati
mbaya matapishi yalimpata aliyekuwa ameketi kando yake akaloa. Huyu alikuwa
msamaria mwema aliyemtendea dada huyu wema. Alimwambia hamna neno na kumpanguza.
Wakati abiria wengi walikuwa wakinung'unika
na kumkashifu dada huyu kwa tendo hilo, huyu msamaria alimjali kwa hali aliyokuwa
nayo. Ni tendo dogo ila ni wachache ambao waweza kujihusisha nalo. Tendo la
kumsaidia mtu mwenza wakati was dhiki ama kwa hali mbayo aliyonayo, si la kawaida
kwa wote.

No comments:
Post a Comment